audio
kitabu cha muundo wa binadamu kwa mtazamo wa kimagharibi (Kaitai Shinsho 解体新書)
Sanaa za Kijapani
dk14 sek55

Siku ya kutangaza Oktoba 1, 2015
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Safari hii kazi ya sanaa inatupelekea mwishoni mwa karne ya kumi na nane katika mji wa Edo, au Tokyo kwa sasa, ambapo kundi la matabibu walipata kitabu kilichoandikwa kwa lugha ya Kiholanzi. Maelezo yaliyokuwemo kuhusu muundo wa mwili wa binaadamu yalitofautiana mno na kile kilichopokelewa nchini Japani kutoka kwenye tiba ya kale ya Kichina. Matabibu hao walishangazwa na kuthibitisha usahihi wa kilichoandikwa kwa kufanya upasuaji. Baadaye wakaamua kukitafsiri kitabu hicho. Ilikuwa kama “kufunga safari baharini kwenye ngalawa bila ya kuwa na kasia wala usukani”. Kitabu hicho cha mfululizo wa vitabu vitano, Kaitai Shinsho – Kitabu cha Muundo wa Binaadamu kwa Mtazamo wa Kimagharibi, kilikamilika katika kipindi cha miaka mitatu na nusu baada ya kazi ya kutafsiri kuanza. Kilikuwa kitabu cha kwanza kuhusu Mtazamo wa Kimagharibi kwenye Muundo wa binaadamu kilichosomwa zaidi ndani ya Japani. Kipindi hiki cha leo kinafuatilia jitihada yao kubwa kwa ajili ya elimu katika zama ambazo mabadilishano na ulimwengu wa nje ya Japani ulikuwa ukidhibitiwa vikali. Hii yote ilitokea takriban miaka mia moja kabla Japani kufungua milango yake kwa ulimwengu.

photo