audio
Pambo la kambamti mwenye miba (Jizai Ise-ebi okimono)
Sanaa za Kijapani
dk12 sek58

Siku ya kutangaza Septemba 17, 2015
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Pambo la kambamti mwenye miba, ni kazi ya sanaa ya mapambo ya chuma inayostaajabisha, iliyoundwa kufanana kabisa na Kambamti halisi. Ni dogo kiumbo kulinganisha na Kambamti halisi, likiwa na urefu wa sentimita 28, ikiwemo sharubu zake. Kiwiliwili, miguu, sharubu na mkia vinasogea kwa uhuru. Modeli zilizotengenezwa kwa chuma ama madini mengineo kama hii zinajuulikana kwa jina la Mapambo yenye viungo na zimekuwa zikitengenezwa nchini Japani tangu mwanzoni mwa karne ya kumi na nane hadi hii leo. Yana viungo vinavyocheza kwa uhuru na yanawakilisha sawia viumbe kama nyoka, mwewe na wadudu wengine. Mifano ya modeli hizo inapatikana katika makumbusho mashuhuri kote duniani. Upekee wake, usawia, na ustaajabu wake unaendelea kuvutia watu duniani kote bila ya kujali utamaduni na enzi.

photo