audio
Kimono aina ya Kosode iliyotengenezwa na kitambaa cheupe chenye mapambo ya mimea na maua ya msimu wa pukutizi (Kosode shiroayaji akikusamoyou)
Sanaa za Kijapani
dk14 sek54

Siku ya kutangaza Septemba 3, 2015
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Uzuri wa vazi la kiasili la wanawake wa Kijapni, “kimono”, unabebwa zaidi na michoro ama mapambo kwenye kitambaa chake. Baadhi huchukuliwa kama kitambaa kizito na mchoraji huchora michoro yake moja kwa moja kwenye kitambaa hicho. Kimono chenye thamani ya kipekee kilichotambulishwa kwenye kipindi hiki kinatoa mfano bora wa mbinu hiyo. Kimechorwa na msanii mashuhuri wa karne ya kumi na nane, Ogata Korin. Kikionyesha maua mwitu ya majira ya pukutizi bila ya mchanganyiko mkubwa wa rangi na muundo wa kawaida inaonyesha vilivyo ubunifu wa kipekee wa Korin. Korin alizaliwa kwenye familia maarufu zaidi ya utengenezaji kimono katika mji wa Kyoto lakini, kwa sababu fulani, alijishughulisha kidogo na ubunifu wa mitindo ya kimono. Alichora kimono hicho baada ya kuhamia kwenye makazi yake mapya ya Edo katika umri wake wa miaka ya 40. Tunaangalia mambo yaliyopelekea kuzaliwa kwa kazii hii ya sanaa, kuanzia mitindo ya wakati huo hadi ujenzi wa mji huo mpya.

photo