audio
Michoro inayoeleza Vita vya wenyewe kwa wenyewe enzi za Heiji: Mviringisho wa nyaraka za taarifa ya ziara ya kifalme kwa eneo la Rokuhara (Heiji Monogatari Emaki, Rokuhara Gyoukou no Maki)
Sanaa za Kijapani
dk15 sek47

Siku ya kutangaza Julai 2, 2015
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Uhamishaji wa Familia ya Kifalme hadi Rokuhara, moja ya Miviringisho ya Nyaraka za Michoro za Hadithi za Vita vya Heiji vya wenyewe kwa wenyewe, una kiasi cha urefu wa sentimita 40 na upana wa takriban mita 9 uliotengenezwa katika karne ya kumi na tatu. Inaonyesha matukio halisi ya karne ya kumi na mbili, ikionyesha ushujaa wa wapiganaji wengi wa samurai katika zama ambazo nguvu zao zilianza kuzishinda zile za mfalme na za tabaka la juu ambazo zilitawala. Miviringisho ya Nyaraka za Michoro iliingizwa Japani kutokea China kwenye karne ya nane hususan kama maandiko matakatifu ya kibudda. Hata hivyo hapa Japani, iliboreshwa kwa namna ya kipekee na kutumika kuelezea hadhithi na habari za aina mbali mbali. Msomaji wa miviringisho hiyo lazima akunjue na kukunja miviringisho hiyo mfululizo ili kuona picha zinazoonekana moja baada ya nyingine kama katuni za anime. Kazi hii ya Sanaa inatumia vizuri mbinu hiyo ya usomaji wa miviringisho ya nyaraka za picha kuonyesha ustadi wa mapigano wa samurai.

photo