audio
Nyumba kwa ajili ya hafla ya chai, Rokusoan (Rokusoan)
Sanaa za Kijapani
dk15 sek30

Siku ya kutangaza Juni 18, 2015
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Nyumba ya hafla ya chai ya Rokusoan katika bustani za Makumbusho ya Taifa ya Tokyo ilijengwa jijini Nara katika karne ya kumi na saba na kujulikana kama moja ya nyumba bora za Nara za hafla ya chai kutokana na ubora kwenye uzuri wake. Ilihifadhiwa ili kuhamishiwa kwenye Makumbusho ya Taifa ya Tokyo katika nusu ya pili ya karne ya kumi na tisa baada ya kuanza kuharibika. Nyumba hiyo ya hafla ya chai ilibomolewa na kusafirishwa kwa meli ambayo ilikumbwa na kimbunga. Meli hiyo iliharibika vibaya lakini kwa bahati nzuri vipande vya nyumba hiyo viliweza kupatikana na kujengwa tena. Ilibomolewa tena ili kuepukana na moto kutokana na mashambulizi ya anga wakati wa Vita Kuu vya Pili vya Dunia na kujengwa tena baada ya vita hivyo kumalizika. Nyumba hiyo ya hafla ya chai ni ndogo na jengo lake halina mapambo kwenye muonekano wake, lakini, katika falsafa ya kipekee ya Japani ya unywaji chai, nyumba ya hafla ya chai ni sehemu maalum ambapo mwenyeji na wageni wake wanaweza kuwa huru, na kukaa pamoja kwa upendo kupitia unyuwaji chai. Uwezo wa hisia za ndani za aliyejenga zinazotokeza kwenye sifa za ubora wa vifaa na nyenzo zilizotumika kwenye kujengea. Na nyumba nyingi kama hizo hurithishwa na kuthaminiwa na vizazi hadi vizazi.

photo