audio
Albamu ya Picha za Kasri la zamani la Edo. (Kyu Edojo Shashinjo)
Sanaa za Kijapani
dk17 sek34

Siku ya kutangaza Juni 4, 2015
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Albamu ya Picha za Kasri la zamani la Edo lilitengenezwa mwaka 1871 mara baada ya Japani kuingia kwenye muelekeo wa zama za usasa. Albamu hiyo ina picha 64 za Kasri la Edo, ambalo lilikuwa ishara ya nguvu za utawala wa Shogun ukoo wa Tokugawa. Tunaona siku za mwisho za zama zilizostawi za samurai katika mandhari iliyokuwa tayari imeanza kubadilika ya Ngome ya Edo na majengo yaliyobakia ambayo yalikuwa yameharibika. Japani ilikuwa inaingia kwenye zama mpya na albamu hiyo ya picha, mbinu mpya ya mawasiriwano wakati huo, ilionyesha baadhi ya mifano ya zamani zaidi ya matumizi ya picha katika kuweka kumbukumbu za tunu za kitamaduni. Ninagawa Noritane, mtayarishaji wa albamu hiyo, aliyekuwa na mtazamo wa kutafakari ya siku zijazo, ndiye aliyeweka kumbukumbu ya tunu hizo kwa ajili ya vizazi vijavyo. Picha hizo alizopiga za namna Ngome ya Edo iilivyoonekana katika enzi zake, sasa zinatumiwa na wasanifu majengo pamoja na wanahistoria.

photo