audio
Barakoa ya Konron iliyochongwa kwa ubao, kwa ajili ya maigizo ya Gigaku (Gigaku Men Konron)
Sanaa za Kijapani
dk14 sek21

Siku ya kutangaza Mei 21, 2015
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Gigaku, Sanaa kongwe zaidi ya maonyesho katika kumbukumbu nchini Japani, inadhaniwa kuwa iliwasili kutoka Kusini Mashariki mwa China katika karne ya saba. Barakoa za mbao za Gigaku zilikuwa zikitumika kwenye maonyesho hayo. Miongoni mwa wahusika wengi walioonyeshwa kwenye sanaa hiyo, tunamuangalia mmoja anaejuulikana kwa jina la Konron. Barakoa ya Konron kwenye barakoa zilizopo kwenye Makumbusho ya Taifa ya Tokyo inaonekana kama pepo baya linalotisha kwa macho yake makubwa yaliyotoka nje, na meno makali yanayochomoza nje ya mdomo wake. Kwenye hadithi ya maonyesho hayo, hata hivyo, mhusika huyo anaonyeshwa kwa njia ya utani kuichekesha hadhira. Utumiaji wa barakoa unaonekana katika tamaduni kote duniani na unaendelea kuwa bado maarufu katika nchi za Asia. Hata hivyo, ni chache tu kati ya barakoa kongwe zimebakia hadi sasa. Barakoa za Gigaku zilitumika kwenye sherehe ya karne ya saba baada ya ukarabati wa hekalu la Horyuji lililoharibiwa na moto na inaaminika kuwa ni barakoa kongwe zaidi za mbao duniani. Asili ya Gigaku bado inaendelea kugubikwa na usiri lakini tunaweza kupata uhusiano utokanao na nchi za mbali.

photo