audio
Kengele ya tambiko ikiwa na mistari (Dotaku)
Sanaa za Kijapani
dk13 sek45

Siku ya kutangaza Aprili 16, 2015
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Kengele za dotaku zilizotengenezwa Japani kuanzia karne ya pili kabla ya kuzaliwa Kristo hadi karne ya tatu baada ya kuzaliwa kwake zinaaminika kuwa zikitumika kwenye matambiko. Kengele hii ya tambiko ikiwa na mistari, inakisiwa kuwa ilitengenezwa karne ya pili ama ya kwanza kabla ya kuzaliwa Kristo. Picha za michoro zilizochorwa kwenye sura yake ni pamoja na ile ya kerengende, kasa mwenye gamba laini na uwindaji wa nguruwe mwitu kwa kutumia mbwa. Michoro ya watu wawili wakitumia mawe ya kusagia nafaka na jengo lenye sakafu iliyonyanyuliwa zinathamani kubwa kwenye kuashiria kuhusu mtindo wa maisha ya watu wa enzi ambazo kilimo cha mpunga kiliingia Japani. Shaba iliyotengenezewa na ustadi wa uhunzi wake, vyote viliingia kwenye visiwa vya Japani kutokea nje, China ama Rasi ya Korea. Kengele za shaba za dotaku zinaonyesha namna wakazi wa enzi za zamani wa Japani walivyopata ustadi wa kigeni na kuugeuza katika njia zao mahsusi.

photo