audio
Birika la chai, Studio ya Ninsei, Mwezi na mti wa plamu unaong'aa (Ninsei "Iroe Getsubaizu Chatsubo")
Sanaa za Kijapani
dk14 sek45

Siku ya kutangaza Aprili 2, 2015
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Birika la Majani ya Chai lenye picha ya mwezi na mti wa mplamu yenye nakshi inayong’aa lilitengenezwa kwenye karakana ya Ninsei katika karne ya kumi na saba. Linaonyesha picha iliyojaa rangi mbali mbali, huku maua ya mplamu yakichanua kwa rangi nyekundu na fedha, na shina na matawi ya mti huo yakiwa na hasa rangi ya kijani na zambarau. Mwezi ni wa rangi ya fedha, na mawingu ya dhahabu yanaelekea huku na kule kwenye mti. Ilikuwa ni vigumu mno kutengeneza kazi yenye muonekano wa picha kwenye ufundi wa ufinyanzi kwa kutumia ubunifu uliokuweko wakati huo. Ubadilishaji wa picha kwenye sura bapa kuwa kwenye umbo la pande tatu la mviringo pia inathibitisha utaalamu wa kipekee wa Ninsei. Birika hilo linasemekana kuwa liliagizwa na Kyogoku Takatoyo, Mbabe wa kivita wa Marugame katika kisiwa cha Shikoku. Takatoyo alikuwa ni kijana mdogo aliyependa picha na aliyetamani Kyoto, mji mkuu wa Japani kwa wakati huo. Ili kutimiza maombi hayo, Ninsei akatoa kazi zake za kipekee. Kyoto enzi hizo ilikuwa mji uliosheheni ubunifu ambapo mawazo mapya ya kisanii yalizalishwa kwa kutumia utaalamu mkubwa.

photo