audio
Miti ya misonobari, kazi ya msanii Hasegawa Tohaku (Hasegawa Tohaku "Shorinzubyoubu")
Sanaa za Kijapani
dk14 sek23

Siku ya kutangaza Februari 5, 2015
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Kazi hii ya sanaa inawakilisha uwepo wa uchoraji wa kijapani wa kutumia wino. Uchoraji huo wa kutumia wino wa rangi moja, unaonesha miti ya misonobari, na kwa nyuma unaonesha milima iliyofunikwa na theluji. Ukiangalia vizuri, kitu kinachoonekana kama michoro ya mistari mingi meusi, kwa mbali kitaonekana kama majani ya miti ya misonobari. Na kwa mbali zaidi, inaonekana misitu ya miti ya misonobali. Kwa juhudi hiyo ndogo, msanii huyo amefanikiwa kuonesha kitu kikubwa chenye manufaa iwezekanavyo, na hata hali ya hewa yenye ukungu.

photo