audio
Wimbi kubwa nje ya pwani ya Kanagawa, kazi ya msanii Katsushika Hokusai (Katsushika Hokusai "Kanagawaoki Namiura")
Sanaa za Kijapani
dk16 sek01

Siku ya kutangaza Januari 22, 2015
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Kazi maarufu ya kisanii ya Japani iliyochangia katika mabadiliko ya sanaa za kisasa za kimagharibi mwishoni mwa karne ya 19. Huo ni wakati ambao kazi nyingi za kisanii za Japani zilianza kuonekana, baada ya Japani kufungua milango kwa mataifa mengine. Hata wakati ambao Japani ilikuwa imejifungia, wasanii wake walijifunza sanaa ya kimagharibi kwa kutumia nyenzo kidogo zilizokuwepo. Uchongaji huu kwenye kipande cha ubao uliofanywa na Hokusai, pia unaakisi alichojifunza kupitia sanaa ya kimagharibi. Kutoka kwenye kazi inayoonesha mawimbi na mlima Fuji, kipindi chetu kitaangazia dhamira ya wasanii wa magharibi na mashariki, katika kubuni muundo mpya wa kupendeza.

photo