audio
Upunguzaji wa Athari za Majanga kwa Wakazi wa Japani kutoka Nje ya Nchi (sehemu ya 1): Wachina na Wabrazil
BOSAI, hatua za kuokoa maisha
dk14 sek34

Siku ya kutangaza Mei 20, 2020
Inapatikana hadi Mei 20, 2021

Mbali na hatari zote za majanga ambazo Japani inakabiliana nazo, wakazi wa Japani kutoka nje ya nchi wamekabiliana na matatizo yao wenyewe katika miaka ya hivi karibuni. Jopo la utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Keio lilifanya utafiti katika jamii mbalimbali ili kufahamu ukweli na kutathmini mahitaji yao. Tutakuletea matokeo ya utafiti huo katika vipindi viwili. Kipindi cha kwanza kitaangazia jamii za raia wa China na Brazil. (Kipindi hiki kilitangazwa Februari 12, 2020.)

photo Wanafunzi wa chuo kikuu wakifanya mahojiano na Duan Yuezhong ambaye anahamasisha mabadilishano kati ya wakazi raia wa China na Wajapani. photo Eneo la mawasiliano kati ya Wajapani na Wachina lipo wazi kila Jumapili katika bustani ya Tokyo. photo Taarifa katika lugha ya Kireno na lugha zingine ilitolewa katika mazoezi ya kukabiliana na majanga katika eneo la Joso mkoani Ibaraki. photo Warsha na Profesa Rajib Shaw wa Chuo Kikuu cha Keio, ambaye ni mtaalam wa kupunguza athari za majanga aliyefanya utafiti huo.