audio
Upunguzaji wa Madhara Yatokanayo na Majanga kwa Jamii zenye Tamaduni Anuai
BOSAI, hatua za kuokoa maisha
dk14 sek31

Siku ya kutangaza Mei 26, 2020
Inapatikana hadi Mei 26, 2021

Mada ya kipindi hiki ni ulindaji katika jamii zenye tamaduni anuai. Tetemeko la ardhi la Great Hanshin lililotokea mkoani Kobe miaka 25 iliyopita lilisababisha kuanza kwa kituo cha redio ya jamii kwa wakazi kutoka nchi zingine. Makundi yanayowakilisha watu wazungumzao lugha mbalimbali pia yamekuwa yakinadi matukio ya BOSAI. Tajiriba na jitihada katika mkoa wa Kobe zinatoa vidokezo vyenye manufaa kwa watu kwingineko duniani. (Kipindi hiki kilitangazwa Januari 16, 2019.)

photo "FMYY" ilianza baada ya tetemeko la ardhi la Kobe mwaka 1995. Roxana Oshiro kutoka jamii ya wanaozungumza Kispanyola, na mafanyakazi wa kujitolea wa Japani wanatoa vipindi vya moja kwa moja vya BOSAI kila wiki katika Intaneti. photo Comunidad Latina Hyogo iliandaa tukio la BOSAI ya Krismasi lililohudhuriwa na wakazi 1,000, Wajapani na wale wenye asili ya Amerika Kusini. photo Shizuyo Yoshitomi (kushoto), profesa wa masomo ya kigeni ya Chuo Kikuu cha Nagoya ananadi suala la utamaduni anuai.