Kampuni ya kutengeneza mvinyo yatumia haidrojeni katika mchakato wa utoneshaji

Kama juhudi ya kuhamasisha kuondokana na kaboni, kampuni ya kutengeneza vinywaji nchini Japani ya Suntory Holdings inasema imefanikiwa kutumia haidrojeni kama fueli katika mchakato wa utoneshaji wa kuzalisha mvinyo. Kampuni hiyo inasema mbinu hiyo imefanikiwa katika msingi wa majaribio, na kwamba inapanga kuanza matumizi ya biashara ya mchakato huo katika kiwanda cha utoneshaji mwaka 2025.

Kampuni hiyo inasema imeanzisha teknolojia ya utoneshaji ili kuzalisha mvinyo bila kupunguza ubora kama vile ladha.