Kishida: Japani italegeza zaidi udhibiti wa mipaka dhidi ya virusi vya korona

Waziri Mkuu wa Japani Kishida Fumio amesema nchi hiyo italegeza zaidi udhibiti wa mipaka unaolenga kuzuia kuenea kwa virusi vya korona.

Kishida aliyasema hayo wakati akiwahutubia wanahabari jijini New York nchini Marekani alikohudhuria Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Kishida alisema Japani itafuta ukomo wa idadi ya watu wanaoingia nchini humo. Pia itaondoa marufuku ya usafiri wa mtu binafsi na kuruhusu ziara zisizohitaji viza kuanzia Oktoba 11.