Qatar kuweka vizuizi vya kuingia nchini humo wakati wa Kombe la Dunia la soka

Wenyeji wa Kombe la Dunia la FIFA, Qatar wametangaza vizuizi kwa watakaozuru nchi hiyo ikionekana wanahakikisha matukio yanafanyika bila tatizo.

Serikali ya Qatar jana Jumatano ilisema kuwa itaanzisha vizuizi hivyo kuanzia Novemba mosi hadi Disemba 22. Mchezo wa Soka utaanza Novemba 20.

Wakati wa kipindi hicho, nchi hiyo itaruhusu kuingia nchini humo raia wa Qatar, raia wa kigeni ambao ni wakazi nchini humo na wenye tiketi ya kutazama mechi za Kombe la Dunia. Wasafiri wa kibiashara na watalii hawataruhusiwa.