Maandamano ya kupinga ukusanyaji wa wanajeshi wa akiba yafanyika kote nchini Urusi

Waandamanaji wameingia mitaani kote nchini Urusi baada ya Rais Vladimir Putin kutangaza kuwakusanya wanajeshi wa akiba jana Jumatano.

Katikati ya jiji la Moscow, vikosi vya usalama viliwakamata na kuwaweka ndani ya magari waandamanaji waliokuwa wakipaza sauti za kupinga vita wakiwa na kauli mbiu zinazopinga ukusanyaji wa jeshi hilo la akiba.

Kundi moja la kutetea haki za binadamu la Urusi limesema watu wasiopungua 1,251 walikamatwa katika miji 38 kufikia jana Jumatano jioni.