Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa: ‘Migawanyiko inakua zaidi’

Katika hotuba yake kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York nchini Marekani, Katibu Mkuu Antonio Guterres alielezea dunia "iliyojaa machafuko."

Guterres aliwakaribisha viongozi kwenye Mkutano wa Baraza Kuu jana Jumanne. Aliwaonya kwamba dunia "iko hatarini na imepooza." Alisema kuwa Mkataba wa Umoja wa Mataifa na itikadi zinazouwakilisha ziko hatarini.

Guterres alisema kuwa migawanyiko na ukosefu wa usawa vinazidi kukua. Aliwataka viongozi kufanya kazi pamoja katika kile alichokiita "muungano wa dunia."

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alijitoa kama "mwezeshaji" katika mazungumzo kati ya Urusi na Ukraine. Alisema vita havitashinda na mchakato wa amani hautakuwa na mshindwa. Pia alisisitiza umuhimu wa diplomasia na kusuluhisha mizozo kwa njia ya mazungumzo.