Kimbunga Nanmadol chageuka kuwa mkandamizo mdogo wa hewa

Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa ya Japani inasema kimbunga Nanmadol leo Jumanne asubuhi kiligeuka kuwa mkandamizo mdogo wa hewa juu ya Bahari ya Pasifiki mashariki mwa Japani.

Kimbunga hicho kilisababisha mvua kubwa katika mkoa wa Miyazaki uliopo kusini magharibi mwa nchi hiyo, ambako maafisa wa hali ya hewa walitoa onyo la dharura la kunyesha kwa mvua kubwa kuanzia juzi Jumapili hadi jana Jumatatu. Mafuriko na maporomoko ya ardhi yametokea.

Watu wasiopungua wawili wamefariki na 122 wameripotiwa kujeruhiwa kote nchini Japani. Mtu mmoja hajulikani aliko.