Mfalme wa Japani na Mkewe wawasili Uingereza kwa ajili ya mazishi ya Malkia Elizabeth

Mfalme Naruhito wa Japani na Mkewe Masako wamewasili jijini London kuhudhuria mazishi ya kitaifa ya Malkia Elizabeth wa Pili. Ibada ya mazishi itafanyika kesho Jumatatu.

Ndege ya serikali iliyowabeba wawili hao iliwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Stansted jana Jumamosi. Baadaye walielekea kwenye hoteli katikati ya jiji hilo.

Wasaidizi wa Mfalme Naruhito wamesema mfalme anazo kumbukumbu nzuri za muda alioutumia pamoja na Malkia Elizabeth, wakati huo Mfalme Naruhito akiwa bado anasoma kwenye Chuo Kikuu cha Oxford katika miaka ya mwanzoni ya 1980.

Malkia alimwalika kuungana naye pamoja na wanafamilia wengine wa kifalme kwenye mandari. Wasaidizi wake wanasema Mfalme Naruhito alimshukuru sana Malkia kwa uchangamfu na ukarimu aliouonyesha kwake.