Waziri Mkuu wa India amtaka Putin atafute amani

Uvamizi wa kijeshi nchini Ukraine umesababisha Rais wa Urusi Vladimir Putin kutengwa na Marekani pamoja na washirika wake. Alilazimika hata kujibu “maswali na wasiwasi” kutoka kwa viongozi wa China. Sasa, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amemkumbusha Putin juu ya jukumu lake duniani.

Viongozi hao walikutana jana Ijumaa kwenye mkutano wa viongozi wakuu wa nchi za kundi la uchumi na usalama wa maeneo liitwalo ‘Shirika la Ushirikiano wa Shanghai.’ Putin alirejelea kwa Modi kile alichomwelezea Rais Xi Jinping wa China juzi Alhamisi.

Alisema, “Ninafahamu msimamo wako katika mgogoro huu wa Ukraine. Ninafahamu kuhusu wasiwasi wako unaouelezea mara kwa mara. Tutafanya kila tuwezalo kumaliza vita hivi mapema iwezekanavyo.”

Modi alitoa wito kwa Rais Putin, ambaye ni rafiki yake wa muda mrefu, kutafuta amani kwa namna yoyote itakayowezekana.

Alisema, “Hii si zama ya vita, na nimezungumza nawe mara nyingi kwa njia ya simu kuhusu suala hili kwamba demokrasia, diplomasia, na majadiliano yataweza kuithibitishia dunia ni kwa namna gani tutaifikia amani katika siku zijazo.