Jeneza la Malkia lawasili kasri la Westminster

Jeneza lililobeba mwili wa Malkia Elizabeth II liliwasili katika Kasri la Westminster jana Jumatano.

Awali, mwili wa Malkia uliondoshwa kutoka Kasri la Buckingham kwa mara ya mwisho. Mfalme Charles III na wanafamilia wengine wa kifalme waliungana na msafara huo. Sare na nembo za walioshiriki zilitumika kama kumbukumbu ya hadhi ya kijeshi ya Malkia.

Justin Welby ambaye ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Canterbury aliongoza misa fupi.

Watu wengi waliofuatilia tukio hilo walisubiri kwa saa kadhaa kuona msafara na kutoa heshima zao za mwisho.

Mwili wa Malkia utawekwa kwenye kasri hilo hadi Jumatatu asubuhi. Askari wa Jeshi la Wanamaji la Kifalme watapeleka jeneza kwenye kanisa la kifalme la Westminster Abbey kwa ajili ya maziko.