Waziri wa Fedha wa Japani hajakataa kuingilia soko ili kuzuia yeni isiporomoke

Waziri wa Fedha wa Japani Suzuki Shunichi hajakataa kuingilia moja kwa kwenye soko ili kuzuia yeni isiporomoke.

Suzuki aliwaambia wanahabari jana Jumatano amekuwa akisema kwamba kasi ya mienendo katika soko la fedha haifai. Alidokeza kuwa kuna uwezekano wa kuyumba kwa sarafu hiyo katika siku chache zijazo, lakini mwelekeo wa jumla ni kushuka thamani yake.

Aidha Suzuki alisema ikiwa mwelekeo huo utaendelea, serikali itachukua hatua zinazohitajika katika soko la fedha kwa namna yoyote ile.

Alipoulizwa kama hatua hizo zitajumuisha uingiliaji wa soko, alisema sahihi kufikiria hivyo.

Kadhalika wanahabari waliuliza iwapo serikali iliingilia kati mapema jana Jumatano.

Suzuki hakujibu, akisema uingiliaji kama huo hautangazwi hadharani. Lakini alisema kama serikali inaamua kuingilia, itafanya hivyo papo hapo.