Mfalme wa Japani na Mke wake kuhudhuria mazishi ya Malkia Elizabeth

Mfalme wa Japani Naruhito na Mke wake Masako watahudhuria mazishi ya kitaifa ya Malkia wa Uingereza Elizabeth II. Mazishi hayo yamepangwa kufanyika Septemba 19.

Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri Matsuno Hirokazu alitoa tangazo hilo leo Jumatano.

Itakuwa ziara yao ya kwanza nje ya Japani tangu Mfalme huyo alipochukua ufalme mnamo mwaka 2019.