Hisa za Tokyo zaporomoka zaidi ya alama 800

Soko la Hisa la Tokyo limeshuka kwa kasi jijini Tokyo leo Jumatano baada ya mauzo makubwa jijini New York jana Jumanne.

Kwa muda mfupi kipimo cha Nikkei 225 kilishuka kwa zaidi ya alama 800 baada ya kipimo cha Dow Jones kupoteza zaidi ya alama 1,200 jana Jumanne.

Mauzo yalichochewa na kipimo cha bei ya mlaji, CPI kuwa juu kuliko ilivyotarajiwa kwa mwezi Agosti nchini Marekani.

Hii imewashawishi wawekezaji kuwa Benki kuu ya Marekani itaendelea kuongeza viwango vya riba, ambavyo vinaweza kupooza uchumi.