Bei za wazalishaji wa Japani zaongezeka kwa mwezi wa 18

Bei za wazalishaji zilipanda nchini Japani kwa mwezi wa 18 mfululizo mnamo mwezi Agosti. Viwanda vililipa zaidi kwa ajili ya malighafi mbalimbali.

Benki Kuu ya Japani inasema gharama za bidhaa zilizouzwa miongoni mwa makampuni ziliongezeka kwa asilimia 9 katika mwezi Agosti kutoka mwaka mmoja uliopita.

Ongezeko hilo ni pungufu ya takriban asilimia 10 iliyorekodiwa mwezi Aprili. Bado ongezeko la mwezi uliopita limebaki kubwa kiasi.

Wasambazaji wa bidhaa wanaendeleza gharama kubwa kwa kuongeza bei za bidhaa zinazouzwa kwa makampuni mengine.

Mgogoro nchini Ukraine na hofu kuhusiana na usambazaji wa mafuta ghafi zimefanya nishati na malighafi kuwa ghali zaidi.

Bei za zaidi ya asilimia 80 ya bidhaa kwenye kipimo zimeongezeka.
Hizi ni pamoja na umeme, chuma cha pua na bidhaa za chakula kama vile vinywaji na ngano.