Mazishi ya Malikia Elizabeth kufanyika Sept. 19 Kanisa la Westminster Abbey

Familia ya Kifalme ya Uingereza imetangaza kwamba mazishi ya kitaifa kwa ajili ya Malkia Elizabeth wa Pili yatafanyika Jumatatu ya Septemba 19 jijini London.

Malkia alifariki dunia akiwa kwenye Kasri la Balmoral nchini Scotland Alhamisi iliyopita.

Familia ya Kifalme ilitangaza jana Jumamosi kwamba mazishi ya kitaifa ya Malkia yataanza saa tano asubuhi mnamo Septemba 19 kwenye kanisa la Westminster Abbey kwenye mji huo mkuu wa nchi hiyo.

Jeneza la Malkia litaondoka kwenye Kasri la Balmoral leo Jumapili. Litawekwa kwenye kanisa kuu mjini Edinburgh kabla ya kupelekwa jijini London siku ya Jumanne.

Siku ya Jumatano, jeneza hilo litapelekwa Ukumbi wa Westminster, ambao ni jengo la zamani kabisa kwenye eneo la Bunge.

Huko, mwili wa Malkia utawekwa katika enzi kwa siku nne kwa ajili ya umma kupata fursa kutoa heshima zake za mwisho.

Mazishi ya kitaifa ya yatafanyika kwenye Kanisa la Westminster Abbey, ambapo sherehe za kifalme za kutawazwa huwa zinafanyikia.

Septemba 19 imetangazwa kuwa mapumziko ya kitaifa.