Mawaziri wa Mpangokazi wa Kiuchumi wa Indo-Pasifiki wakutana Los Angeles Marekani

Mawaziri kutoka nchi 14, ikiwemo Japani, Marekani na India wanakutana Los Angeles nchini Marekani kwa ajili ya mkutano wao wa kwanza wa ana kwa ana leo Alhamisi chini ya mpango mpya kwa ajili ya Indo-Pasifiki.

Marekani ilipendekeza Mpangokazi wa Kiuchumi wa Indo-Pasifiki kwa ajili ya Ustawi, yaani IPEF huku ushawishi unaoongezeka wa China katika eneo hilo.

NHK ilipata rasimu ya taarifa ya pamoja itakayotolewa katika mkutano huo wa siku mbili.

Moja ya mihimili minne ya majadiliano ni mtungo wa usambazaji thabiti wa bidhaa muhimu kama semikondakta.

Washiriki watajadili namna ya kutengeneza mpangokazi utakaowezesha kujiandaa na hali ikiwa usambazaji wa bidhaa za semikondakta, rasilimali na chakula utasitishwa.

Chini ya mpangokazi huo, kila nchi wanachama itaweka mratibu ambaye atashirikishana taarifa juu ya nchi zinazokumbwa na uhaba wa bidhaa fulani.

Mihimili iliyobaki inajumuisha majadiliano juu ya kanuni za biashara za viwango vya juu ikiwemo matumizi ya teknolojia ya kidijitali.

Aidha washiriki wanalenga kuandaa taarifa ya kila mhimili kwa lengo la kutangaza rasmi kuanza kwa majadiliano.