Kundi linaloiunga mkono Urusi lashukiwa kufanya udukuzi katika tovuti za serikali ya Japani

Serikali ya Japani inasema kundi la udukuzi linaloiunga mkono Urusi linashukiwa kufanya kile kinachofahamika kama shambulio la DDoS kwenye mtandao wa serikali.

Idara ya Kidigitali inasema mifumo kadhaa ya serikali inaaminika kushambuliwa kutoka nje ya nchi jana Jumanne mchana. Kiwango kikubwa cha data kimepelekwa kwa shambulio la DDoS ili kufanya tovuti hizo kutopatikana.

Kuingia katika baadhi ya tovuti hizo kulitatizika jana Jumanne ikiwemo “e-Gov” ambayo inatoa taarifa za kiutawala.

Kundi la udukuzi linaloiunga mkono Urusi linaloitwa Killnet lilituma ujumbe kwenye mtandao wa kijamii jana Jumanne wa kudai kuhusika na shambulio hilo.

Kundi hilo pia lilitumia mbinu ya DDoS katika udukuzi wake kwenye mataifa mengine.