Wakaguzi wa IAEA wasalia kwenye mtambo wa Zaporizhzhia, mashambulizi yakiendelea

Timu ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki, IAEA ilizuru mtambo mkubwa zaidi barani Ulaya ili kupunguza hofu ya uwezekano wa kutokea janga. Wengi wa wakaguzi hao walimaliza kazi zao huku wakaguzi wawili wakisalia kwenye mtambo wa Zaporizhzhia nchini Ukraine jana Jumatatu. Mashambulizi makali ya makombora hayajasitishwa.

Mtambo huo umedhibitiwa na wanajeshi wa Urusi tangu siku za kwanza za uvamizi. Maafisa wa kampuni ya nyuklia ya serikali ya Ukraine ya Energoatom walitangaza kuwa njia ya hifadhi ya mwisho inayounganisha mtambo huo kwenye gridi ya nishati ya Ukraine imekatwa. Wanasema moto uliosababishwa na makombora uliharibu njia hiyo. Rais wa kampuni hiyo Petro Kotin alisema timu ya IAEA inapaswa kuongoza usitishaji wa Urusi kudhibiti mtambo huo.

Kotin alisema, “Inapaswa kuwa zaidi ya ‘kuhofu.’ Inapaswa kuwa njia ya namna ya kutatua masuala yote yaliyopo sasa kwenye eneo hilo.”

Alitoa wito kwa timu zingine za kimataifa kuzuru mtambo huo, wakiwemo walinda amani wa Umoja wa Mataifa.