Japani yaitikia vikali hatua ya Urusi kufuta makubaliano ya visiwa vinne

Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri la Japani Matsuno Hirokazu amewaambia wanahabari leo Jumanne kwamba hatua ya Urusi si ya haki kabisa na haikubaliki.

Amesema serikali imewasilisha malalamiko makali kwa Urusi licha ya kutopokea taarifa kutoka kwa nchi hiyo.

Kadhalika Matsuno alisema Urusi inawajibikia kwa hali ya sasa ya uhusiano wa Japani na Urusi, unaofanya isiweze kufanya mabadilishano kati ya wakazi wa zamani wa Japani na wakazi wa sasa wa Urusi wa visiwa hivyo vinne.