NASA kupitia kuahirishwa tena kwa urushaji wa roketi kwenda mwezini

Shirika la Anga za Juu la Marekani, NASA limesema kwamba litaangazia kubaini matatizo ya msingi baada ya kulazimika kwa mara nyingine tena kuahirisha kurushwa kwa roketi ya kisasa inayobeba chombo kisichoendeshwa na rubani kwenda kwenye mzingo wa dunia.

NASA ilifuta jaribio lake la hivi karibuni la kuirusha roketi hiyo jana Jumamosi. Ni uahirishwaji wa pili kufanyika katika juma moja. Awali urushaji huo ulipangwa ufanyike Jumatatu wiki hii kwenye Kituo cha Anga za Juu cha Kennedy kilichopo kwenye jimbo la Florida.

Shirika hilo lilisitisha zoezi hilo la jana Jumamosi kutokana na kuvuja kwa kimiminika cha fueli ya haidrojeni kutoka kwenye injini ya roketi.

Mfumo wa Kisasa wa Anga za Juu wa Kurushia roketi umetengenezwa kwa ajili ya programu ya Artemis, mradi wa kimataifa wa kuchunguza mwezi unaolenga kuwapeleka wanaanga kwenye uso wa mwezi kufikia mwaka 2025. Kapsuli mpya ya Orion ya NASA imepachikwa kwenye roketi hiyo.

Artemis ni jaribio la kwanza kupeleka wanaanga kwenye mwezi tangu mpango wa Apollo wa mwishoni mwa miaka ya 1960 na mapema 1970. Japani na baadhi ya nchi za Ulaya ni miongoni mwa washiriki kwenye jitihada hizo zinazoongozwa na Marekani.

Maafisa wa shirika hilo walisema urushwaji mpya unatarajiwa kufanyika kwenye nusu ya pili ya mwezi huu ikiwa ni mapema zaidi.