Japani na Uingereza kupanga kwa pamoja kutengeneza bodi ya ndege ya kivita

Wizara ya Ulinzi ya Japani inafanya utaratibu kushirikiana na Uingereza katika kutengenza kwa pamoja bodi ya ndege mpya ya kivita.

Kampuni kubwa za Kijapani na Uingereza zilianza utafiti mwezi Januari mwaka huu wa kutengeneza kwa pamoja injini mpya ya ndege ya kivita itakayochukua nafasi ya ndege aina ya F-2 za Kikosi cha Kujihami cha Anga cha Japani.

Nchi hizo mbili tayari zimekubaliana kuandaa mpango juu ya namna zitakavyoshirikiana katika kutengeneza ndege hiyo mpya kufikia mwishoni mwa mwaka. Ratiba iliandaliwa pale mawaziri wakuu wa nchi hizo mbili walipokutana mwezi Mei mwaka huu.

Wizara ya ulinzi inaamini utengenezaji huo wa pamoja utasaidia kupunguza gharama kutokana na mahitaji mahsusi kwa ndege hizo ambayo Japani na Uingereza zinatahitaji ni karibu yanafanana.

Italia pia inaangaziwa kama mshirika atakayeongezwa na Japani kutokana na nchi hiyo tayari inashirikiana na Uingereza katika utengenezaji wa ndege za kivita.

Wizara ya Ulinzi ya Japani imejumuisha yeni bilioni 143.2, ama takribani dola bilioni moja, kutengeneza ndege mpya za kivita kwenye ombi la bajeti iliyotengwa kwa mwaka ujao wa fedha.

Inatumai kuanza kuwa na mrithi wa F-2 tayari hadi pale kufikia wakati watakapoacha kuzitumia ndege hizo, karibu na mwaka 2035.