Jiji la Chengdu nchini China laweka amri ya kutotoka nje

Jiji la Chengdu nchini China limetangaza marufuku ya kutotoka nje kufuatia kuenea kwa virusi vya korona.

Maafisa katika jiji hilo lililopo jimbo la Sichuan wanasema walirekodi zaidi ya visa 700 vya virusi hivyo kati ya Agosti 25 na 31. Jiji hilo lina idadi ya takribani watu milioni 21.

Maafisa hao walianzisha marufuku ya kutotoka nje kwa siku nne jijini kote kuanzia jana Alhamisi usiku, wakielezea hofu kwamba virusi hivyo vinaweza kuenea zaidi. Wanawataka wakazi wa jiji hilo kufanya vipimo vya PCR katika kipindi hicho.

Hii ni marufuku ya kwanza kuwekwa kwa jiji nchini China tangu hatua kama hiyo kutekelezwa kote jijini Shanghai kwa zaidi ya miezi miwili kuanzia mwishoni mwa mwezi Machi.