UAE kutoa viza za utalii kwa walio na tiketi za Kombe la Dunia la Soka nchini Qatar

Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE umesema utatoa viza za utalii kwa watu walio na tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia la FIFA la mwaka 2022, ambalo litaanza Novemba katika nchi jirani ya Qatar.

UAE ilisema katika taarifa yake jana Jumatano kwamba viza za kuingia mara nyingi zitatumika kwa muda siku 90.