Urusi yaruhusu kampuni ya Mitsui & Co. kusalia na hisa katika Sakhalin-2

Serikali ya Urusi imeidhinisha uamuzi wa kampuni ya biashara ya Japani ya Mitsui & Co. kudumisha hisa zake katika mradi wa mafuta na gesi wa Sakhalin-2 katika Mashariki ya Mbali ya nchi hiyo.

Katika amri iliyotangazwa jana Jumanne, Urusi ilisema inaruhusu kukabidhi asilimia 12.5 za hisa katika kampuni mpya iliyoanzishwa na kuchukua utekelezaji wa mradi huo.

Asilimia hiyo ni sawa na hisa ambazo Mitsui ilikuwa nazo kwa mwendeshaji wa zamani.

Mapema mwezi Agosti, Urusi iliziambia kampuni za Mitsui & Co. na Mitsubishi Corporation kwamba zilihitaji kuamua ndani ya mwezi mmoja ikiwa zilitaka kuwa na hisa katika kampuni mpya. Kampuni zote mbili zimeamua kuchukua hisa.