Maswali na Majibu: Usalama wa viyoyozi na feni (3)

(3) Matarajio ya kudumu kwa bidhaa

NHK inajibu maswali yanayohusiana na kuhakikisha usalama katika maisha ya kila siku. Nchini Japani, hatuna budi ila kutegemea viyoyozi na feni za umeme kuepuka ugonjwa wa kuzirai kutokana na joto kali wakati wa miezi yenye joto kali wakati wa msimu wa joto. Lakini uzee na saa nyingi za kuendelea kuvitumia kunaweka mzigo kwa vifaa hivi na kusababisha ajali kwa mfano kushika moto. Katika kipengele hiki, tunaangazia hatari zinazowekwa na viyoyozi na feni na kukupatia vidokezo vya kuvitumia kwa usalama. Leo hii, tunaangazia matarajio ya kudumu kwa bidhaa.

Viyoyozi na feni za umeme zimekuwa na uwezekano mkubwa wa kupatwa na ajali baada ya muda fulani kutokana na kuchakaa kwa sehemu zake. Hivyo imeilazimu serikali kuwaagiza watengenezaji kuainisha “kipindi cha matumizi cha msingi kulingana na utengenezaji wake.” Ukiwekwa na kila mtengenezaji, urefu wa muda ambao kifaa kinaweza kutumika kwa usalama bila matatizo chini ya utumiaji wa kawaida unaonyeshwa katika sehemu inayoonekana kwenye kila bidhaa. Taasisi ya Taifa ya Teknolojia na Tathmini inawashauri watumiaji kutumia kipindi hiki kama mwongozo wa kubadilisha, na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa kila bidhaa inayotumiwa baada ya kupita kipindi hiki. Iwapo hali isiyo ya kawaida itabainika, taasisi hiyo inawashauri watumiaji kuzima kifaa hicho mara moja na kuwezesha kukaguliwa na mtengenezaji na kadhalika.

Taarifa hii ni sahihi hadi kufikia Julai 11, 2024.