Kim Jong Un ahudhuria ibada ya kumbukumbu ya babu yake

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amehudhuria ibada ya kumbukumbu ya kuadhimisha miaka 30 tangu kufariki kwa babu yake Kim Il Sung anayechukuliwa kama mwasisi wa taifa hilo.

Runinga ya serikali ya Korean Central iliripoti kuwa tukio hilo lilifanyika jana Jumatatu katika Uwanja wa Kim Il Sung mjini Pyongyang.

Kim alihudhuria ibada hiyo akiwa amevalia suti nyeusi. Afisa mwandamizi wa chama tawala cha Wafanyakazi alitoa hotuba akipongeza urithi wa mamlaka kwa vizazi vitatu. Afisa huyo alisema ni utamaduni wa kipekee wa Korea Kaskazini kwamba itikadi ya kiongozi inarithishwa katika njia safi zaidi na bora zaidi.