Mkuu wa MSDF aripotiwa kunuia kujiuzulu kutokana na utunzaji mbovu wa taarifa za siri

Wizara ya Ulinzi ya Japani ilisema inaangazia kuwakemea viongozi waandamizi wa Kikosi cha Kujihami cha Majini cha Japani, MSDF kufuatia taarifa kwamba waliruhusu wafanyakazi wasiostahili kushughulikia taarifa za siri. Mnadhimu mkuu wa MSDF Admiral Sakai Ryo ameripotiwa kuelezea nia yake ya kujiuzulu.

Mwezi Aprili, wizara hiyo ilimsimamisha kazi kapteni wa manowari ya MSDF, ikisema afisa huyo alimruhusu mfanyakazi asiyestahili kushughulikia “siri maalumu zilizotengwa,” zikiwemo baadhi ya zinazohusiana na meli ya kigeni.

Vyanzo vya habari vinasema uchunguzi wa wizara ulibaini kulikuwa na visa kama hivyo, kama vile kwenye manowari zingine nyingi.

Wanasema Admiral ameelezea nia yake ya kutaka kujiuzulu.

Wizara inatarajiwa kutangaza matokeo ya uchunguzi wake na mfanyakazi atakayepewa karipio mapema mwezi huu.