Kamanda mwandamizi wa Hezbollah auawa katika shambulio la Israel

Kundi la Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Lebanon, Hezbollah limetangaza kuwa shambulizi la jeshi la Israel limemuua mmoja wa makamanda wake wandamizi jana Jumatano.

Hezbollah ililipiza kisasi kwa kurusha roketi kuelekea Israel.

Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant aliripotiwa kusema kuwa Israel "itafikia hali ya kuwa tayari kabisa kuchukua hatua zozote zinazohitajika nchini Lebanon. Tunapenda mazungumzo lakini kama ukweli ndo utatulazimisha tutajua namna ya kupigana."

Hali bado ya wasiwasi, kwani mapigano makali kati ya pande hizo mbili yanahofiwa kuzuka.

Jeshi la Israel pia jana Jumatano lilitangaza kwamba mashambulizi yake "yametokomeza magaidi" kusini na kaskazini mwa Gaza.