Ofisi ya rais wa Urusi: Putin na Xi kukutana nchini Kazakhstan

Ofisi ya rais wa Urusi inasema Rais Vladimir Putin leo Jumatano atakutana na mwenzake wa China Xi Jinping nchini Kazakhstan.

Msaidizi wa rais Yury Ushakov alitangaza jana Jumanne kwamba viongozi hao wawili watakutana pembezoni mwa mkutano wa Shirika la Ushirikiano wa Shanghai unaofanyika katika nchi hiyo ya katikati mwa Asia.

Inaaminika kuwa Urusi inatumai kuthibitisha tena ushirikiano wake na China katikati ya mgogoro unaoendelea na Ulaya na Marekani juu ya hali nchini Ukraine.

Mkutano huo uliopangwa kati ya Putin na Xi unafuatia mazungumzo yao yaliyofanyika mwezi Mei, ambapo walikubaliana kuimarisha zaidi uhusiano wao wa kiuchumi na kupanua kiwango cha mazoezi ya pamoja ya kijeshi.