Bei za bidhaa 411 za vyakula na vinywaji zitapanda mwezi Julai

Bei za bidhaa 411 za vyakula na vinywaji zinatarajiwa kupanda mwezi Julai, kutokana na udhaifu wa yeni, gharama za usambazaji na mambo mengine.

Kampuni binafsi ya utafiti ya Teikoku Databank ilichunguza watengenezaji wakubwa 195 wa vyakula na vinywaji kote nchini Japani.

Karibu nusu ya bidhaa hizo ni vileo na vinywaji vinavyoagizwa kutoka nje kama vile mvinyo, wiski na bidhaa za kahawa. Bei ya mkate pia itapanda, pamoja na bidhaa za chokoleti na asusa, kutokana na kupanda kwa bei ya mbegu za kakao.

Bei za vyakula 10,086 zinatarajiwa kupanda kuanzia Januari hadi Novemba mwaka huu, ikiwa ni mwaka wa tatu mfululizo kwa idadi hiyo kufikia 10,000.

Kampuni hiyo ya utafiti inasema bidhaa zaidi zinapanda bei tena kutokana na gharama za juu za uagizaji kutoka nje ya nchi zinazotokana na kushuka zaidi kwa thamani ya yeni. Inatarajia bei ya hadi takriban bidhaa 15,000 za vyakula kupanda ifikapo mwisho wa mwaka.