China inatekeleza sheria kwa ukaguzi wa vifaa vya kielektroniki kutokana na hofu ya ujasusi

China inatekeleza sheria mpya leo Jumatatu inayoruhusu mamlaka za usalama wa taifa kukagua vifaa vya kielektroniki kutokana na shutuma za ujasusi.

Wizara ya Usalama wa Taifa inatekeleza sheria hiyo inayotoa mamlaka ya kukabiliana na ujasusi.

Sheria hiyo inatoa taratibu za kukagua simu za mkononi, kompyuta binafsi na vifaa vingine vya watu binafsi na mashirika.

Inatoa wito kwa maafisa kuunda taarifa kwa idhini kutoka kwenye mamlaka za usalama wa taifa katika ngazi ya manispaa ama juu ya manispaa.

Lakini sheria hiyo inawaruhusu maafisa kufanya ukaguzi katika hali za dharura ikiwa wana idhini na kuelezea mamlaka yao.

Wizara hiyo inasisitiza kuwa sheria hiyo inanuiwa kuzuia shughuli haramu zinazohatarisha usalama wa taifa.

Wachambuzi wanasema mamlaka zitatumia sheria hiyo kusisitiza kuwa ukaguzi wao ni halali.