Japani kutoa takwimu za hali ya hewa kwa visiwa vya Pasifiki

Serikali ya Japani inapanga kutoa takwimu za hali ya hewa kwa visiwa vya Pasifiki Kusini ili kuvisaidia kukabiliana na majanga.

Tangazo la mpango huo litatolewa katika mkutano wa 10 wa viongozi wakuu wa visiwa vya Pasifiki uliopangwa kuanza Julai 16 hadi 18 jijini Tokyo.

Tangu mwaka 1997, Japani imewaalika viongozi wa Pasifiki Kusini katika mkutano mara moja kila baada ya miaka mitatu. Viongozi 18 wanapanga kuhudhuria mkutano wa mwaka huu na Waziri Mkuu Kishida Fumio atakuwa mwenyekiti mwenza.

Kishida anapanga kutangaza kuwa Japani itatoa takwimu za Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Japani. Taarifa hizo zitatumika kwa ajili ya uokozi na hatua zingine katika matukio ya majanga kama vile vimbunga na tsunami.

Takwimu hizo zitatolewa kwa wakati sahihi kwa kutumia satelaiti ya Michibiki, mfumo wa Kijapani wa uongozaji kwa satelaiti wa GPS.

Takwimu hizo zitatolewa kwanza kwa kisiwa cha Fiji kama mradi wa majaribio.

Katika miaka ya hivi karibuni, China imekuwa ikiongeza ushawishi kwenye visiwa vya Pasifiki Kusini kupitia miradi ya miundombinu.

Japani inapanga kuimarisha uhusiano na mataifa katika eneo hilo kwa kusaidia njia zao za kukabiliana na majanga kuongezea na miaka mingi ya msaada rasmi ya maendeleo.

Waziri mkuu wa Japani pia anatarajiwa kuelezea umwagaji maji yaliyotibiwa kutoka katika mtambo wa nyuklia wa Fukushima Namba Moja ulioharibika na kutoa wito wa uelewa wa usalama wake.

Mtambo wa nyuklia wa Fukushima Namba Moja uliyeyuka mara tatu katika tetemeko la ardhi na tsunami la mwaka 2011.

Maji yaliyotumika kupooza fueli iliyoyeyuka yamekuwa yakichanganyika na maji ya mvua na ya ardhini. Maji yaliyokusanywa yanatibiwa ili kuondoa dutu za mionzi hatari, lakini bado yana tritiyamu.

Kabla ya kuyaachia baharini maji yaliyotibiwa, mwendeshaji wa mtambo huo anayapooza ili kupunguza viwango vya tritiyamu hadi takribani moja ya saba ya kiwango cha mwongozo cha Shirika la Afya Duniani kwa ajili ya maji ya kunywa