Wizara ya afya ya Japani imepiga marufuku uuzaji wa bidhaa 14 zenye dutu kama bangi

Wizara ya afya ya Japani jana Ijumaa ilitoa agizo la kupiga marufuku uuzaji wa bidhaa 14 ambazo zina dutu karibu sawa na bangi katika maduka ya nchi nzima na mtandaoni.

Maafisa wa wizara wanasema visa viwili vya madhara ya afya viliripotiwa mwezi Aprili mwaka huu. Watu walio na umri wa miaka ya 20 walikimbizwa hospitalini baada ya kula bidhaa zinazoaminika kuwa na dutu kama za bangi aina ya HHCPM na kujisikia kusinzia.

Visa hivyo vilisababisha wizara ya afya kufikiria kuwa ni muhimu kudhibiti uzalishaji na usambazaji wa bidhaa hizo.

Agizo la wizara hiyo lilifanya jumla ya bidhaa zilizopigwa marufuku kufikia 58.

Maafisa wanazingatia kudhibiti dutu katika bidhaa kama dawa zilizoainishwa.