Mvua kubwa eneo la Kyushu huenda ikasababisha maporomoko ya ardhi

Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa nchini Japani inasema kuwa hewa ya unyevunyevu na joto inayoelekea kwenye mpaka baina ya hewa baridi na unyevunyevu na mfumo wenye mgandamizo mdogo katika maeneo ya Kyushu na Tokai inafanya hali za angahewa magharibi na mashariki mwa Japani kutokuwa thabiti kabisa.

Maeneo ya Kyushu, Shikoku na Tokai yamekuwa yakifunikwa na mawingu ya mvua mara kwa mara.

Tahadhari ya kutokea maporomoko ya matope imetolewa katika baadhi ya maeneo mkoani Kagoshima.

Mamlaka hiyo inaonya kuwa kuna uwezekano kwamba hatari ya kutokea kwa janga ikaongezeka ghafla, kwani matabaka ya mawingu ya mvua yanayotarajiwa kujiunda leo Ijumaa asubuhi katika mikoa ya Fukuoka, Oita na Kumamoto yatasababisha kuendelea kwa mvua kubwa.

Tahadhari imetolewa juu ya kutokea kwa maromoko ya matope, mafuriko katika maeneo ya mabondeni na mito kujaa maji au kufurika. Maafisa wa hali ya hewa pia wanaonya juu ya uwezekano wa kutokea kwa radi na pepo kali.