Mfalme wa Japani aweka shada la maua kwenye kaburi la Malkia Elizabeth II na Mwana Mfalme Philip

Mfalme wa Japani Naruhito ameweka shada la maua kwenye kaburi la Malkia Elizabeth II na mumewe, Mwana Mfalme Philip.

Mfalme Naruhito alisafiri kuelekea kanisa la St. George lililopo katika Kasri la Windsor jirani na London jana Alhamisi. Yeye na Mkewe Masako walialikwa rasmi nchini Uingereza na Mfalme Charles.

Mfalme Naruhito aliripotiwa kutamani mno kwenda kanisani hapo walikozikwa Malkia Elizabeth na Mwana Mfalme Philip waliofariki mwaka 2022 na 2021 mtawalia.

Aliwaambia wanahabari kuwa alitembelea kaburi hilo kuonyesha shukrani zake za dhati kwa yote waliomtendea.