Yeni yauzwa na kununuliwa kwa kiwango cha katikati ya yeni 160 dhidi ya dola jijini Tokyo

Kwenye soko la kubadilisha fedha la Tokyo leo Alhamisi, yeni inauzwa na kununuliwa katika kiwango cha katikati ya 160 dhidi ya dola.

Wadau wa soko wanazidi kupata wasiwasi juu ya uwezekano wa kuingiliwa kwa soko na serikali ya Japani na Benki Kuu.

Waziri wa Fedha Suzuki Shunichi alisema leo Alhamisi asubuhi kwamba wizara yake itatathmini kwa uangalifu kinachosababisha yeni kuzorota na kuchukua hatua stahiki.

Kauli hiyo ilisababisha baadhi ya wawekezaji kununua tena sarafu ya Japani.