Vijana wa Kijapani wamepungukiwa na kujiamini

Utafiti wa serikali unaonesha kwamba asilimia 57 ya vijana wa Kijapani wana hisia chanya kuwahusu, ikiwa ni ongezeko la zaidi ya alama 10 kutoka miaka mitano iliyopita.

Alama hizo ni za chini miongoni mwa mataifa matano ambayo uatafiti huo ulifanyika.

Vijana nchini Japani, Marekani, Ufaransa, Ujerumani na Uswidi walishirikishwa katika utafiti huo.

Nchi zote nne za kimagharibi zilipata zaidi ya asilimia 70. Ufaransa ilikuwa na alama za juu zaidi ikiwa na 76.

Utafiti huo wa mtandaoni ulifanyika kuanzia Novemba hadi Disemba mwaka jana miongoni mwa vijana wenye umri wa kati ya miaka 13 hadi 29. Ulifanyika kwa mara ya kwanza nchini Japani mwaka 2013 na kufanyika tena mwaka 2018.

Ni asilimia 23 tu ya washiriki nchini Japani walijibu kwamba nchi yao ina wakati ujao mzuri, punguo la alama 8 kutoka miaka mitano iliyopita.

Karibu asilimia 50 hadi 60 ya walioshiriki kutoka katika nchi zingine nne walitoa maoni chanya kwa swali hilo.

Serikali ya Japani inataka kubadili mtazamo wa vijana kupitia kuboresha sera juu ya umasikini, elimu na ajira.