Mvua kubwa yatabiriwa kote mashariki na magharibi mwa Japani

Mvua kubwa inatabiriwa kunyesha katika maeneo makubwa ya magharibi na mashariki mwa Japani mwishoni mwa juma hili. Mamlaka zinawasihi watu kuchukua tahadhari kwa maporomoko ya ardhi na mafuriko.

Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Japani inasema mpaka wa mvua za msimu wake na mfumo wa shinikizo la chini la hewa zinatarajiwa kuelekea kaskazini hadi kesho Jumapili, hivyo kuongeza hatari ya kunyesha mvua kubwa na radi.

Kwa kipindi cha saa 24 hadi Jumapili asubuhi, mvua za hadi milimita 200 zinatabiriwa kaskazini mwa eneo la Kyushu, 150 kusini mwa eneo la Kyushu, milimita 120 kwenye eneo la Chugoku na milimita 100 kwenye maeneo ya Kinki na Shikoku.

Mamlaka zinasema kuwa janga lilisababisha ardhi kulegea, na hata mvua kidogo zinaweza kusababisha maporomoko ya ardhi.